Ndejembi mgeni rasmi fainali Kihenzile Cup 

FAINALI za Kombe la Kihenzile zimepangwa zitafanyika kesho Jumamosi Desemba 10 katika uwanja wa Igowele S/M
Akizungumza na HabariLEO, Mbunge wa Mufindi Kusini, David Kihenzile ambae ndio mdhamini wa mashindano hayo amesema, fainali hizo zitaanza saa 10 jioni na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi.
Amesema viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya Wilaya na Mkoa watakuwepo.
Aidha wadau mbalimbali wa Sekta ya Michezo na Maendeleo pia watashiriki katika fainali  hizo.
Zawadi mbalimbali zitatolewa kwenye makundi ya mpira wa miguu, Netiball, kukimbiza Kuku, Kuvuta Kamba, Nyimbo za Asili na Ufaulu Darasa la saba.
Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *