Ndizi ‘Moshi’ zaadimika sokoni

NDIZI aina ya mshale, malindi na mnyenyele zinazotoka mkoani Kilimanjaro zimeadimika mkoani Dar es Salaam.

Mfanyabiashara wa siku nyingi katika soko la Ndizi la Urafiki mkoani Dar es Salaam, Gasper Mushi alisema kupungua kwa ndizi hizo maarufu kama ndizi Moshi, kunasababishwa na baridi iliyopo kipindi hiki mkoani Kilimanjaro.

“Soko la ndizi ni shida hasa kutoka Kilimanjaro, kipindi hiki wilayani Moshi ni baridi, huwa zinachukua muda kukomaa.” “Kwa sasa hivi mshale hautoshelezi watu wanakula bukoba zaidi,” alisema.

Advertisement

Alisema kwa sasa ndizi nyingi zinatoka mkoani Mbeya na Bukoba, ambazo ni ndizi bukoba na mzuzu. Alisema kutokana na uchache huo wa ndizi kutoka Kilimanjaro, kwa sasa yanaingia magari matatu au manne sokoni hapo, kwa kila gari linakuwa na mikungu 50 hadi 100.

Alisema kipindi cha ndizi nyingi hufikia mikungu 200 mpaka 250 kwa gari moja, huanza Novemba mpaka Mei. Kwa maelezo yake, kipindi hiki magari ya ndizi yanayotoka Mbeya na Bukoba yanaingia kuanzia saba

5 comments

Comments are closed.