Ndoa ya Bayern, Tuchel kuvunjika Juni

KOCHA mkuu wa vigogo wa soka wa Ujerumani Bayern Munich, Thomas Tuchel ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Vyombo vya habari nchini Ujerumani vinaripoti kuwa baada ya majadiliano yanayotokana na matatizo ya klabu hiyo katika siku za hivi karibuni, FC Bayern na meneja huyo wa zamani wa Chelsea wameamua kuachana mwezi Juni.

“Tumekubaliana kwamba tutamaliza ushirikiano wetu baada ya kumalizika kwa msimu huu. Hadi wakati huo, mimi na wafanyakazi wangu bila shaka tutaendelea kufanya kila tuwezalo kuhakikisha mafanikio ya kiwango cha juu,” Thomas Tuchel amethibitisha.

Advertisement

Bayern watatafuta meneja mpya na tayari kocha na mchezaji wa zamani wa Mancheter united Ole Gunnar Solskjaer, meneja wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso pamoja na kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane wanatajwa kama mbadala wa kuwanoa The Bavarians. Thomas Tuchel atatafuta chaguzi za kazi mpya katika kipindi cha miezi 3 hadi minne 4 ijayo.