Ndolezi ashauri nguvu zaidi kwenye teknolojia

Apendekeza ikibidi teknolojia ifuatwe ughaibuni

DAR ES SALAAM: WAZIRI Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Vijana, Kazi na Ajira wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndolezi Petro amesema kuna haja ya serikali kuwekeza zaidi kwenye eneo la teknolojia hasa kwa vijana.

Soma pia: https://habarileo.co.tz/ndolezi-kunahitajika-baraza-la-vijana-la-taifa/

Akizungumza na HabariLEO mapema leo alipofanya ziara yake katika ofisi za Daily News Digital iliyo chini ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Samora Dar es Salaam, Ndolezi amesema kukua kwa teknolojia kumerahisha vitu vingi katika masuala mbalimbali ikiwemo mawasiliano na usafari.

“Na ikiwezekana twende tukaichukue hiyo teknolojia kwenye nchi ambazo zimepiga hatua tukijifungia kwa kusema tutaharibu kizazi badala yake tutatengeneza kizazi kilichopo kwenye giza,” amesema Ndolezi.

Akizungumzia hoja ya Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo ambaye wiki iliyopita akiwa bungeni jijini aliiomba serikali kuwekeza katika kuwalinda vijana dhidi ya ukuaji wa teknolojia na kwamba isipokuwa makini huenda vijana wakathirika zaidi, amesema:

Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7MPMCWOBoR/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

“Ni muhimu kuwekeza kwenye teknolojia maana yake tusipofanya hivyo tutaingia kwenye mtego ambao hatuufahamu ila ukiwekeza watakuwa na uwezo,” amesema Ndolezi.

Habari Zifananazo

Back to top button