NEC yatahadharisha wasimamizi wa uchaguzi

TUME  ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewakumbusha Wasimamzi wa Uchaguzi kutekeleza wajibu wao kwa kuhakikisha kwamba ajira za watendaji wa uchaguzi zinazingatia sifa na uwezo.
Ukumbusho huo umefanywa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk mkoani Morogoro leo tarehe 10 Agosti, 2023 wakati akifunga mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku tatu na kuhudhuriwa na washiriki 88 ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara.
“Tunayo imani kuwa mtateua na kuajiri watendaji wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi hii muhimu, jambo hili limekuwa likisisitizwa tokea siku ya kwanza ya mafunzo kwa kuwa hao ndio watakaosimamia zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura vituoni;…..”Kazi ambayo inahitaji umahiri, umakini na weledi katika kuitekeleza,” amesema Jaji Mbarouk.
Amesisitiza juu ya kuhakikisha mafunzo kwa watendaji wa vituo vya kupigia kura yanafanywa kwa ufanisi ili wawe na uelewa na kuweza kufanya kazi zao kwa usahihi na kujiamini.
 “Ni imani yetu kuwa mafunzo ya watendaji wa vituo yatafanyika kwa ufanisi na weledi katika tarehe zilizopangwa kwenye ratiba ya utekelezaji wa shughuli za uchaguzi. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo ili waweze kufahamu majukumu yao na kuyatekeleza ipasavyo wakati wa uchaguzi,” amesema Jaji Mbarouk.
Aidha, amewahimiza watendaji wa uchaguzi kutenga muda kujisomea ili kupata ufahamu wa sheria, kanuni na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
“Natumia nafasi hii kuendelea kuwasisitiza kuhusu umuhimu wa kutenga sehemu ya muda wenu kusoma Katiba, Sheria na Maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ili yawaongoze katika kusimamia uchaguzi utakaokuwa huru na wa haki,” amesema.
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara utafanyika tarehe 19 Septemba, 2023, wagombea watachukua fomu kuanzia tarehe 13 hadi 19 Agosti, 2023, siku ya uteuzi itakuwa tarehe 19 Agosti, 2023 na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 20 Agosti, 2023 hadi tarehe 18 Septemba, 2023.
Kata zitakazofanya uchaguzi mdogo ni; Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, mkoani Dodoma, Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi na Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
10 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
bestakeknu
bestakeknu
1 month ago

I earn 200 dollars per hour working from home on an online job. I never thought I could accomplish it, but my best friend makes $10,000 per month doing this profession and that I learn more about it.
.
.
.
For Details►—————————➤ https://fastinccome.blogspot.com/

worldremit
worldremit
Reply to  bestakeknu
1 month ago

money

mapinduzi.PNG
JeanBrown
JeanBrown
1 month ago

Single Mom With 4 Kids Lost Her Job But Was Able To Stay On Top By Banking Continuously DOLLER 1500 Per Week With An Online Work She Found Over The Internet… 

Check The Details HERE…..  https://webonline76.blogspot.com/

Last edited 1 month ago by JeanBrown
worldremit
worldremit
Reply to  JeanBrown
1 month ago

money

mapinduzi.PNG
RebekahShanna
RebekahShanna
1 month ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. x134 Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. q12 Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by. follow instructions on
this website…………> http://www.SmartCash1.com

Last edited 1 month ago by RebekahShanna
worldremit
worldremit
Reply to  RebekahShanna
1 month ago

money

mapinduzi.PNG
worldremit
worldremit
1 month ago

Job Opening

Posting Title:     PROGRAMME MANAGEMENT OFFICER, P4

Job Code Title: PROGRAMME MANAGEMENT OFFICER

Department/Office:      WorldRemit’s

Duty Station:     Tanzania

Posting Period: 31 August 2023 – 21 September 2023

Job Opening Number:  23-Programme Management-WR-212982-R-TANZANIA (X)

Staffing Exercise              N/A

Apply Now

https://careers.worldremit.com/lbw/home.aspx?viewtype=SJ&vacancy=All

worldremit
worldremit
1 month ago

money

mapinduzi.PNG
eventsnikazi eventsnikazi
eventsnikazi eventsnikazi
1 month ago

MONEY

MAPINDUZI.GIF
eventsnikazi eventsnikazi
eventsnikazi eventsnikazi
1 month ago

gharama za kitamba cha green house for sale

MAPINDUZI.GIF
Back to top button
10
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x