NEC yateua Mbunge Viti Maalum

DAR ES SALAAM; TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteua Aziza Ally Sleyum kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima imeeleza kuwa hatua hiyo inatokana na kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge ikiitaarifu Tume kuhusu kuwepo nafasi ya wazi ya ubunge kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Bahati Ndingo.

Bahati alijiuzulu nafasi  hiyo ya ubunge Agosti 17 mwaka huu ili kuwania ubunge katika Jimbo la Mbarali, baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Francis Mtega kufariki dunia Julai Mosi, mwaka huu kwa ajali.

 

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button