Neema yatangazwa kwa wabunifu

DAR ES SALAAM: Shirikisho la Sanaa za Ufundi na Ubunifu limesema Serikali ina mikakati ya kupeleka wabunifu nje ya nchi kwa lengo la kukuza uchumi na kuleta fedha za kigeni nchini.

Akizungumza na HabariLeo Rais wa shirikisho hilo Adrian Nyangamale, aliwataka wabunifu kuongeza ubunifu wa kazi zao ili masoko yao yakatangazwe katika soko la Dunia.

“Tanzania ipo katika uchumi wa kati ambapo watu wake wana fedha na mtu mwenye fedha anapenda kuvaa vizuri hivyo wabunifu waendelee kubuni kwa lengo la kupata fedha na kutangaza masoko yao ndani na nje ya Nchi.”amesema

Pia ameongeza kuwa wabunifu wanapobuni mavazi wazingatie mila na desturi za Watanzania hata wanapoenda kimataifa wanazidi kutangaza utamaduni wa Tanzania nasio wa mataifa mengine

Habari Zifananazo

Back to top button