Neema yawashukia wakulima wadogo

WAKULIMA wadogo wametangaziwa neema, baada ya Shirika la Private Agricultural Sector Support Trust (PASS) na benki ya Finca Microfinance kusaini mkataba wa kuwawezesha wakulima wadogo kupata  mikopo kwa riba nafuu isiyo na dhamana.
Mkataba huo wa miaka miwili unalenga kuwanufaisha wakulima zaidi ya 120,000.
Wakizungumza jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Pass Trust Yohane Kaduma na Mkurugenzi wa Benki ya Finca Microfinance, Edward Talawa walisema makubaliano hayo waliyoingia yatasaidia wakulima wadogo kufanya Kilimo biashara kwa njia ya Kidijitali.
Mkurugenzi wa Finca Edward Talawa amesema “Mikopo hii ya Kilimo itapatikana kwa haraka na unafuu mkubwa kwa sababu itakua ya Kidijitali. ” Amesema
Amesema, tayari wakulima zaidi ya 120,000 wamesajiliwa kupitia vikundi vyao wataweza kuomba na kupata mikopo hiyo kupitia simu zao za mkononi.
“Mikopo hii haitakua huduma ya kwanza ya mikopo Kidijitali kutolewa na benki ya Finca, ila itakua ni huduma ya kwanza na ya kipekee ya mikopo ya Kidijitali inayolenga kukuza na kuendeleza Kilimo.” Amesema Tawala
Nae, Mkurugenzi wa Pass Trust, Yohane Kaduma amesema Mikopo hiyo inalenga kuwanufaisha wakulima wengi wa Tanzania ili kuweza kufikia malengo ya serikali ya kuwainua wakulima wadogo na kupunguza umaskini.
Amesema, Finca ni miongoni mwa benki 14 ambazo wanamakubaliano nazo ya kuwahudumia wakulima wadogo nchini.
Kaduma amesema tangu kuanzishwa Pass Trust miaka 22 iliyopita,  imewezesha mikopo kwa wajasiriamali zaidi ya  zaidi ya  milioni 3.4 yenye thamani ya Shilingi Trilioni 1.43.
“Kati ya wanufaika wote asilimia 46 ni wanawake, jumla ya biashara zipatazo 63,156 zinazojihusisha na mazao na huduma za Kilimo katika kuongeza mnyororo wa thamani zimenufaika na dhamana hizi.” Amesema

Habari Zifananazo

Back to top button