Neema yazidi kufunguka miundombinu ya barabara

Serikali imesaini mikataba mitano ikijumuisha mkataba wa ujenzi wa barabara ya TAMCO – Vikawe hadi Mapinga kwa kiwango cha lami; sehemu ya Pangani hadi Mapinga, ambayo itagharimu zaidi ya shilingi Bilion 500 kwa ufadhili wa serikali na Benki ya Dunia.

Miradi hiyo, minne ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya usafiri wa wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam na mradi mmoja ni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya TAMCO – Vikawe hadi Mapinga.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema ujenzi wa barabara hizo zitasaidia kupunguza foleni na zitawapatia wananchi ajira pindi ujenzi huo utakapoanza .

Naye Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), Mohamed Besta amesema barabara ya  TAMCO vikawe hadi pangani yenye urefu wa Km.13 ni kiungo kati ya Dar es salaaam na Kilimanjaro pamoja na Tanga.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kawe Josephat Gwajima, akataka maeneo ambayo mkandarasi atakayejenga barabara hizo kuzingatia miundombinu ya madaraja katika maeneo korofi.

Habari Zifananazo

Back to top button