Nelly Kamwelu awaza uongozaji filamu

DAR ES SALAAM: MUIGIZAJI maarufu nchini Nelly Kamwelu amesema mbali na sanaa hiyo ana ndoto ya kuwa mwongozaji wa filamu mkubwa Afrika, Kamwelu ambaye ni mshindi wa taji la Miss Southern Africa international 2011 nchini Zambia ameiambia HabariLEO.

Kamwelu ambaye pia aliwahi kuibuka mshindi wa nne taji la ‘Miss Tourism Queen International’ nchini China amemwambia mwandishi wa mtandao huu kuwa sanaa ya uigizaji imempa elimu ya kutosha ambayo itafanya kufikia ndoto hiyo.

SOMA: Mrembo ajipanga kuwashika mkono wahitaji

Mwigizaji huyo ambaye ni mhitimu wa chuo cha uigizaji cha New York Film Academy cha nchini Marekani ameeleza baada ya kutimiza ndoto hiyo hapo ndipo atakuja na kazi yake binafsi ya uigizaji.

Muigizaji Nelly Kamwelu (kushoto) sanjari na muigizaji mwenza na muongozaji wa filamu, Jacob Steven

“Nimejifunza mambo mengi sana kwa sababu hiyo imeniletea mawazo mapya na ari ya kazi. Licha ya kazi ya kuigiza nina ndoto kuwa mwongoza filamu na hapo ndipo nitapanga kuja na mradi wangu binafsi,” ameeleza Kamwelu.

Kamwelu amewahi kushinda taji la Miss Southern Africa international pia kushinda taji la Miss Universe Tanzania mwaka 2011, lakini pian kuibuka mshindi wanne taji la Miss Tourism Queen International’ nchini China.

Habari Zifananazo

Back to top button