NEMC: Gari inayosambaa mitandaoni haituhusu

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limesema halihusiki na gari lenye kava ya tairi yenye nembo ya NEMC likiwa limeegeshwa eneo lisilo rasmi likipatiwa huduma ambalo linaendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Taarifa iliyotolewa leo Aprili 15, 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka imesema kuwa NEMC haina uhusiano wowote na video wala gari inayoonekana.

“NEMC inatumia njia mbalimbali katika kujitangaza ikiwemo kuandaa na kusambaza kava za matairi (wheel covers) zenye jumbe wa mazingira kwa wadau wake, magari yote ya NEMC yana namba za usajili na hufanyiwa matengenezo (service) katika gereji iliyoingia Mkataba wa kisheria wa kutoa huduma husika”

Dk Gwamaka amesema kuonekana kwa gari hilo lenye kava ya tairi lenye nembo ya NEMC haimanishi kuwa gari hilo linamilikiwa na baraza.

Habari Zifananazo

Back to top button