BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewataka wananchi kuacha uvuvi haramu ili kufanya mazingira ya bahari kuwa salama.
Meneja wa NEMC Kanda ya Temeke, Arnold Mapinduzi amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Utunzanzi wa Mazingira (TEEMO) Kanda Kigamboni.
Alisema kwa kuacha uvuvi haramu, kutasaidia mazingira ya bahari kuwa salama na hivyo kuendelea kuzalisha rasilimali mbalimbali zinazopatikana majini.
“Bahari inazalisha hewa safi kwa viumbe, hivyo wananchi wanapaswa kuitunza kwa njia mbalimbali ikiwemo kuacha uvuvi haramu,”alisema
Aliongeza kuwa na hewa safi pia kutawezesha kuzalishwa kwa viumbe wengi na hivyo kusaidia kupatikana mavuno mengi baharini.
Naye Mkurungenzi TEEMO, Winfrida Shonde alisema wanajisikia faraja kuendelea kushiriki pamoja na kutoa elimu juu ya uhifadhi wa mazingira.
“Tuna kauli mbiu zetu,soma mti,okoa dunia na ile ya bahari safi jukumu langu,hivyo ni wajibu kila mwananchi kuendelea kutunza mazingira ili yatutunze,”alisema