Nenda kawafundishe na wengine!
MWANZA; Magu. Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Inspekta Hosiana Mushi, akitoa elimu ya usalama barabarani na kumpongeza dereva bodaboda kwa kuwa mfano bora wa kufuata sheria za usalama barabarani.
–
Amempongeza pia kwa kujali maisha ya abiria wake kwa kumvalisha kofia ngumu, pia alimpongeza kwa kutii amri ya askari kwa kusimamishwa ili akaguliwe, wakati baadhi ya bodaboda wakisimamishwa wanakimbia.