Netanyahu arejea madarakani Israel

WAZIRI Mkuu wa zamani wa Israel Benjamin Netanyahu amerejea madarakani Alhamisi Nov. 3 baada ya uchaguzi wa wiki hii kumpa yeye na washirika wake wa mrengo mkali wa kulia kura nyingi za wabunge.

Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yalisema kuwa kutokana na asilimia 99 ya kura kuhesabiwa, chama cha Netanyahu cha mrengo wa kulia –Likud kimeshinda viti 32 katika bunge la Israel lenye viti 120.

Hilo likijumlishwa na viti 18 kwa vyama viwili vya Wayahudi wenye imani kali ya Kiorthodoksi na viti 14 kutoka muungano unaokua wa mrengo wa kulia unaoitwa Uzayuni wa Kidini ulioipa kambi hiyo inayomuunga mkono Netanyahu viti vingine 64.

Vyama vinavyomuunga mkono Waziri Mkuu wa kwanza Yair Lapid vilishinda viti 51, ushindi ambao unamaanisha mwisho wa enzi ya mkwamo wa kisiasa wa Israeli, ambao ulilazimisha chaguzi tano katika chini ya miaka minne.

Waziri huyo wa zamani wa mrengo wa kulia amesimamia mashambulizi mengi dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi. Saa chache baada ya ushindi wake kuthibitishwa, jeshi la Israel lilishambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza baada ya wapiganaji wa Kipalestina kurusha roketi nne kuelekea Israel.

Mmoja alinaswa na wengine watatu “kulipuka ndani ya ukanda wa Gaza”, jeshi la Israel lilisema, na kuthibitisha uvamizi wa kwanza kutoka eneo hilo tangu mzozo wa siku tatu mwezi Agosti kati ya Israel na kundi la Islamic Jihad. Hakuna kundi lililodai mara moja kuhusika na shambulio la Alhamisi.

 

Habari Zifananazo

Back to top button