MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima amesema Jeshi la zimamoto limefanikiwa kudhibiti moto katika Hoteli ya New Mwanza na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na taratibu kubaini chanzo cha moto huo ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya madhara.
New Mwanza Hoteli, ambayo ipo katikati ya jiji la Mwanza iliripotiwa kuungua moto Agosti 31.