loader
Picha

Maafisa Jeshi 104 Wahukumiwa Kifungo Cha Maisha Jela Uturuki.

Mahakama nchini Uturuki imewahukumu maafisa jeshi 104 kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika jaribio la kupindua serikali ya nchi hiyo mwaka 2016.

Inaelezwa kuwa jaribio hilo lilishindwa kumng’oa madarakani Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan na badala yake kusababisha vifo vya watu zaidi ya 260 na majeruhi 2,200, Julai 15 ya mwaka huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), chombo cha habari cha taifa hilo kimeeleza kuwa hukumu hiyo imetolewa na masharti makubwa zaidi kuliko hukumu nyingine dhidi ya mapinduzi ya serikali.

Rais Erdogan amewahi kunukuliwa akisema serikali italiomba bunge la nchi hiyo kurejesha adhabu ya kifo dhidi ya watakaokutwa na hatia ya uhalifu huo.

KATIKA maeneo mengi nchini watu wamekuwa wakiishi kwa amani na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi