loader
Picha

Waziri aagiza watoto walioungana wakatenganishwe Muhimbili

SERIKALI imetoa mwito kwa jamii nchini kote kuwa popote watakapozaliwa watoto wenye maumbile tofauti au walioungana viungo vya mwili, wafi kishwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH), kuonana na madaktari bingwa ili kuona jinsi ya kuwatenganisha mapema au kupewa huduma bora zaidi.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (Chadema).

Lyimo alitaka kujua kama serikali ina taarifa juu ya watoto waliozaliwa wameungana huko Misenyi katika mkoa wa Kagera na inachukua hatua gani. Ummy alisema, serikali inajua na imemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuwasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ili kuwasafirisha na kuwafikisha Muhimbili ili watenganishwe.

Akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi (Chadema) aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa wajawazito ili wafike kliniki kutokana na asilimia yao ndogo kufika kliniki.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile alisema, idadi ya wanawake wanaofika kliniki mara moja katika kipindi cha ujauzito wanafikia asilimia 90.

“Lakini idadi ya wanawake wanaofika kliniki mara nne katika kipindi cha ujauzito wao wanafikia asilimia 60,” alisema. Dk Ndugulile alitoa rai kwa wajawazito kufika kliniki mara nne katika kipindi cha ujauzito wao ili wapate huduma mbalimbali zikiwemo za mama na mtoto.

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Zubeda Hassan Sakuru(Chadema) aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani kukabiliana na vifo vya watoto wanazaliwa kabla ya wakati. Dk Ndugulile alisema, watoto wanaozaliwa kabla ya wakati au wenye uzito pungufu chini ya kilo 2.5 huwa katika hatari zaidi ya kupoteza maisha kuliko wengine.

KATIKA maeneo mengi nchini watu wamekuwa wakiishi kwa amani na ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi