Msanii Salum Mohamed 'Sam wa Ukweli' amefariki alfajiri ya kuamkia leo baada ya kuzidiwa alfajiri ya kuamkia leo wakati akiwa studio, taarifa kutoka jijini Dar es Salaam zinathibitisha.

Meneja wa msanii huyo, Amri Athuman amethibitisha taarifa hiyo leo asubuhi.

Msanii huyo alipata umaarufu baada ya kutoa kibao chake kilichofahamika kama "Hata Kwetu Wapo."

Mtandao huu wa HabariLeo, Daily News na SpotiLeo inaendelea kufuatilia kwa kina juu ya msiba huo katika tasnia ya burudani.