loader
Picha

Sumu kuimba na Diamond, Kiba

MSANII wa muziki wa singeli, Msaga Sumu amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa yupo katika harakati za kuomba kolabo na wasanii Diamond na Ali Kiba. Akizungumza na mtandao wa Bongo Five alisema kuwa muda ukifika atachagua msanii wa kufanya naye kolabo kati ya wawili hao.

Ipo siku na muda, uzuri sijawaambia wakanikatalia, kila kitu ni mipango naweza nikawaambia nataka kolabo, wakikataa basi hivi vitu havina ulazima,”alisema Msaga Sumu.

Alisema kuwa wasanii wote wawili anawaamini kuwa watafanya vizuri kama ataamua kuimba nao kwani wote ni wasanii waliokulia mazingira ya uswahilini kama muziki huo unavyojieleza. Pia alisema kuwa yeye ndiye mwazilishi wa muziki wa singeli ingawaje kuna baadhi ya watu wanapinga suala hilo kwa kwa madai ya kuwa ni mziki wa kihuni.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo (pichani) amesema wamesafi ri umbali ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi