loader
Picha

Tarimba aanza mkwara Yanga

SIKU moja baada ya wanachama wa klabu ya Yanga kumkabidhi Abbas Tarimba, majukumu ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya kusimamia masuala ya mikataba ya wachezaji na usajili kiongozi huyo ametamba kuwabakisha mshambuliaji Obrey Chirwa na beki Kelvin Yondani.

Baaba ya sintofahamu ya muda mrefu ndani ya klabu hiyo iliyopelekea kuvuruga amani na mafanikio iliyokuwa nayo timu hiyo msimu uliopita, hatimaye juzi Jumapili wanachama wa klabu hiyo walikutana na kufikia makubaliano ya klabu hiyo kubadilisha uendeshwaji wake kutoka ilivyo sasa na kuwa Kampuni ili kunusuru hali hiyo isijirudie siku zijazo.

Mabadiliko hayo pia yalipewa baraka na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe aliyehudhuria kwenye Mkutano huo ambao baadhi ya ajenda zake ilikuwa ni kujaza nafasi zilizokuwa wazi baada ya baadhi ya viongozi kujiuzulu.

Akizungumza na gazeti hilii, siku moja baada ya uteuzi huo, Tarimba alisema majukumu hayo ameyapokea kwa mikono miwili na atajitahidi kutuliza presha za mashabiki wa timu hiyo kwa kuwabakiza nyota wawili waliomaliza mikataba Yondani na Chirwa.

“Ni majukumu mazito, lakini nimeyapokea kwa mikono miwili nitajitahidi kwa kushirikiana na wenzangu kuhakikisha wachezaji hao wanabaki Yanga na pia tunasajili wachezaji wenye uwezo na viwango bora ili kuirudisha timu yetu kwenye ushindani,” alisema Tarimba.

Kiongozi huyo ambaye aliwahi kuiongoza Yanga miaka ya nyuma akiwa Mwenyekiti wa kuchaguliwa na Wanachama alisema yeye na viongozi wenzake wameufurahia Mkutano huo kwa sababu umerudisha amani iliyoanza kupotea ndani ya klabu hiyo ambayo inaongoza kwa mafanikio Tanzania.

Alisema chini yake amedhamiria kumaliza kila kitu kuhusiana na usajili ndani ya mwezi mmoja na nusu na hilo linawezekana kutokana na mgawanyo wa majukumu waliopeana lengo likiwa ni kumaliza haraka iwezekanavyo na kuifanya Yanga irudi kwenye heshima iliyokuwa nayo huko nyuma.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo (pichani) amesema wamesafi ri umbali ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi