loader
Picha

'Simba inaweza kusajili mchezaji yeyote Afrika'

KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imesema itafanya usajili wa kishindo kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu Bara 2018/19.

Akizungumza kwenye tuzo za Mo Simba Dar es Salaam, Kaimu rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Tray Again’ alisema mwekezaji wao amemwambia yuko tayari kumsajili mchezaji yeyote Afrika.

“Simba inakwenda kusajili kwa kishindo, mwekezaji ameniambia yupo tayari kumsajili mchezaji yeyote Afrika, kwa hiyo tuna matumaini ya kufanya vizuri zaidi msimu ujao,” alisema.

Simba ipo kwenye hatua za mwisho za kubadili mfumo wa uendeshaji kuingia kwenye utaratibu wa hisa ambapo mfanyabiashara na mwanachama wa klabu hiyo Mohamed ‘Mo’ Dewji ndiye mnunuzi wa hizo asilimia 49 dhidi ya 51 za wanachama.

Mpaka sasa Simba haijaanza kufanya usajili wa wachezaji wa kimataifa, imesajili wachezaji wawili wa ndani na kumuacha wa kimataifa mmoja, Laudit Mavugo aliyemaliza mkataba wake.

Aidha, Salim aliwapongeza wachezaji wake kwa kupambana kutwaa taji la Ligi Kuu na kwamba kupoteza mechi ya fainali dhidi ya Gor Mahia kwenye fainali za SportPesa Super Cup wiki iliyopita ni jambo la mpira.

“Hongera kwa wachezaji mmepambana na kutwaa taji la Ligi Kuu, kwa bahati nzuri pia tumefika fainali za SportsPesa lakini kwa bahati mbaya tumepoteza, hiyo ndio soka… mpambane msikate tamaa,” alisema.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo (pichani) amesema wamesafi ri umbali ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi