loader
Picha

Bin Kleb aitisha Simba

MJUMBE wa Kamati maalumu ya kushughulikia usajili na mikataba wa klabu ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, amesema kurejea kwake kundini kunaashiria kumalizika kwa zama za utawala wa watani zao, Simba.

Jumapili iliyopita wanachama wa Yanga, waliunda kamati maalumu itakayohusika na mambo mbalimbali ikiwemo suala la usajili ambapo aliyewahi kuwa Mweyekiti wao Abbas Tarimba alipewa uongozi wa kamati hiyo yenye wajumbe 10.

Bin Kleb aliwahi kuwa kwenye Kamati hiyo siku za nyuma na ‘umafia’ wake uliiweka katika wakati mgumu Simba kwenye usajili kwani ndiye aliyemsajili beki Mbuyu Twite na kiungo Haruna Niyonzima na kuifanya Yanga kung’ara misimu kadhaa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Bin Kleb aliwashukuru wanachama wa Yanga kwa kuonesha imani kwake na kuahidi kupambana kwa ajili ya kujenga kikosi bora kitakachorudia mafanikio.

“Mimi niwashukuru wanachama wa Yanga kwa imani yao kwangu lakini kingine niwape salamu watani zetu Simba, wajue nimerudi kazini na nitafanya zaidi ya ilivyokuwa kipindi hicho ilimradi Yanga ipate kila mchezaji aliyekuwa na ubora wa kuifanya irudi kwenye kiwango chake,” alisema Bin Kleb.

Mjumbe huyo alisema Yanga haina tatizo la fedha za usajili kama ambavyo watu wanadhani na kwa kulithibitisha hilo wasubiri kuona baada ya mkutano huo kwamba watanunua mchezaji wanayemtaka bila kujali gharama yake kutokana na ushawishi pamoja na fungu waliloweka katika usajili.

Alisema kwa walipopanga kwenda hatarajii kuona Simba wakaingilia kati tena usajili wao kama ilivyokuwa kwa washambuliaji Mohamed Rashid, Marcel Kaheza na Adam Salamba ambao wao ndio waliokuwa wakwanza kutangaza kuwasajili lakini Simba wakawapiku na kumalizana nao.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo (pichani) amesema wamesafi ri umbali ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi