loader
Picha

Jengo la Beit-al-Jaib lakarabatiwa

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wamejulishwa kwamba ukarabati wa jengo la Beit-Al-Jaib umeanza chini ya ufadhili mkubwa Serikali ya Oman.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo wakati akitoa ufafanuzi mbele ya wajumbe kuhusu maendeleo ya ukarabati wa jengo hilo baada ya kutiwa saini makubaliano hayo Mascut, Oman.

Alisema ukarabati wa jengo hilo utahusisha sehemu mbalimbali muhimu ikiwemo paa la nyumba hiyo ambalo lilivujiwa kwa muda mrefu na kuruhusu maji kuingia ndani.

Aidha, alisema ukarabati wa jengo hilo utawahusisha wajenzi wazalendo zaidi ambao ni wale wenye uzoefu wa kujenga kwa kutumia mawe na mchanga.

Alisema jengo hilo litatumia kwa kiasi kikubwa mawe na mchanga kwa sababu ndiyo asili yake pamoja na kutekeleza masharti ya miji iliyopo katika urithi wa kimataifa.

“Napenda kuwajulisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba tumeanza kazi za ukarabati mkubwa wa jengo la Beit-Al-Jaib chini ya ufadhili wa ndugu zetu wa Oman, ambao utafanyika hatua kwa hatua chini ya maelekezo na masharti ya Mamlaka ya Hifadhi ya Mji Mkongwe,'' alisema.

Alisema matengenezo ya jengo hilo ni muhimu kwa sababu limebeba historia kubwa ya Zanzibar pamoja na watawala mbalimbali waliotawala Zanzibar hadi Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 mwaka 1964.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi