loader
Picha

Vigogo sita wa Bodi ya Mikopo watumbuliwa

Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imewaachisha kazi watumishi sita wa bodi hiyo kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kushindwa kutimiza majukumu yao. 

Watumishi hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Urejeshaji wa Mikopo Juma Chagonja, Mkurugenzi wa Upangaji na Ugawaji Mikopo Onesmus Laizer, Mkurugenzi Msaidizi wa Ugawaji Mikopo John Elias na Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo, Robert Kibona.

Wengine ni Heri Sago ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Hesabu, pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Upangaji Mikopo Chikira Jahari.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Mwenyekiti wa bodi hiyo, Profesa William Anangisye, maamuzi hayo yamefikiwa kupitia kikao cha bodi kilichokaa Juni 22, baada ya watumishi hao kusimamishwa kazi kati ya mwaka 2016 na 2017 kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali dhidi yao.

Watumishi hao wameachishwa kazi kwa makosa tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na kushindwa kutekeleza majukumu yake ya urejeshaji wa mikopo kwa mujibu wa Kanuni na Taratibu za urejeshaji wa Mikopo.

MKUTANO wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa ...

foto
Mwandishi: Na Janeth Mesomapya

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi