loader
Picha

Watatu Simba wawania tuzo VPL

MABINGWA wa Ligi Bara msimu wa mwaka 2017/18 Simba wametoa wachezaji watatu wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa ligi hiyo.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) , Cliford Ndimbo amesema jijini Dar es Salaam kwa, kamati ya tuzo imepitisha majina matatu kuwania tuzo ya mchezaji bora ambao ni Emmanuel Okwi, John Bocco na Erasto Nyoni.

“Wachezaji Emmanuel Okwi, John Bocco na Erasto Nyoni wote wa Simba ndio waliopendekezwa kuwania tuzo ya mchezaji bora pia kamati imeandaa utaratibu wa kupiga kura kuwashirikisha wahariri wa habari za michezo, manahodha na makocha wa timu za Ligi Kuu,” alisema Ndimbo.

Aidha, kamati hiyo hiyo iliyo chini ya mwenyekiti Ahmed Mgoyi, imetaja wachezaji watakaowania tuzo katika vipengele mbalimbali.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Juni 23 mwaka huu, Mlimani City Dar es Salaam.

Tuzo 16 zinatarajiwa kutolewa siku hiyo, ambapo baadhi ni za kikanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, ambazo tayari washindi wake wamefahamika, ambazo ni bingwa, mshindi wa pili, mshindi wa tatu, mshindi wa nne na mfungaji bora.

Tuzo zingine 10 ambazo zimefanyiwa kazi na kamati hiyo kulingana na takwimu za ligi ni mchezaji bora chini ya umri wa miaka 20 (Tuzo ya Ismail Khalfan), inayohusisha vikosi vya vijana vya timu za Ligi Kuu ambayo kwa sasa inaendelea Dodoma na itakapokamilika watatangazwa wateule watatu.

Tuzo nyingine zitakazotolewa siku hiyo ni timu yenye nidhamu inayowaniwa na Kagera Sugar, Simba na Mtibwa Sugar, wakati Mchezaji Bora Chipukizi inawaniwa na Shaaban Chilunda, Yahya Zayd (Azam) na Habibu Kiyombo (Mbao).

Tuzo ya mwamuzi bora msaidizi inawaniwa na Helen Mduma, Mohammed Mkono na Ferdinand Chacha, wakati Mwamuzi Bora wateule ni Elly Sasii, Jonesia Rukyaa na Hance Mabena.

Tuzo ya Kipa Bora wanaowania ni Aron Kalambo (Prisons), Aishi Manula (Simba) na Razack Abalora (Azam), huku Kocha Bora wateule ni Abdallah Mohamed (Prisons), Zuberi Katwila (Mtibwa) na Pierre Lechantre (Simba). Goli bora ni Seif Karihe (Lipuli) na Chilunda (Azam) ambaye ameingiza mabao mawili.

Tuzo nyingine ambazo zitatolewa ni ya mchezaji wa heshima ambayo licha ya kuwa kamati ina majina ya wachezaji mbalimbali inaoona wanastahili tuzo kwa mwaka husika, lakini haitangazi majina hayo, isipokuwa hutaja jina la aliyepewa tuzo siku ya sherehe.

Pia kutakuwa na kikosi bora (VPL Best Eleven), ambacho kitatangazwa siku ya sherehe.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo (pichani) amesema wamesafi ri umbali ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi