loader
Picha

Umasikini wapungua Tanzania

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema, kiwango cha umasikini nchini kimepungua kutoka 28.2% mwaka 2011/2012 hadi asilimia 24.6 mwaka 2015/2016.

Amewaeleza wabunge kuwa, Serikali ina mpango wa kupunguza kiwango cha umasikini hadi asilimia 16.7 mwaka 2020 na 12.7% ifikapo mwaka 2025.

Amesema bungeni jijini Dodoma kuwa, mwaka 2017 pato la wastani la kila mtu lilikuwa shilingi 2,275,601 ambazo ni sawa la Dola za Marekani 1021.

Ameyasema hayo wakati anawasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2017 na Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Kwa mujibu wa Waziri Mpango, mwaka 2017 pato halisi la taifa lilifikia shilingi trilioni 50.5.

Amesema, mwaka jana uchumi wa dunia ulikua kwa wastani wa asilimia 3.7.

Dk Mpango amesema, mwaka 2016 uchumi wa dunia ulikua kwa asilimia 3.1.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameagiza ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi