loader
Picha

Tanzania yaongoza kasi ya uchumi EAC

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema, mwaka 2017 uchumi wa Tanzania ulikua kwa kasi zaidi kuliko wa nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Waziri Mpango, mwaka jana uchumi wa Tanzania ulikua kwa wastani wa asilimia 7.1.

Amewaeleza wabunge kuwa, mwaka jana uchumi katika nchi za Afrika Mashariki ulikua kwa wastani wa asilimia 1.9.

Amesema, kasi ya ukuaji uchumi Tanzania ilifuatiwa na ya Rwanda (6.1%), Kenya (4.8%), Uganda (4.5%), Burundi (0.0%), na ule wa Sudan Kusini ulipungua kwa asilimia 11.1

“Uchumi wa nchi hizi unatarajiwa kuendelea kukua kwa kasi zaidi kufikia wastani wa asilimia tatu nukta sita mwaka 2018” amesema wakati anawasilisha taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa na Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka 2018/2019.

Kwa mujibu wa Waziri Mpango, wastani wa kasi ya ukuaji wa uchumi kwa nchi za Afrika Kusini ya Jangwa la Sahara ilikuwa asilimia 2.8.

Amewaeleza wabunge kuwa mwaka 2016, uchumi kwenye eneo hilo ulikua kwa kasi ya asilimia 1.4.

“Matarajio ni kufikia wastani wa asilimia 3.3 mwaka 2018. Matarajio hayo ya ongezeko la ukuaji wa uchumi yametokana na kuongezeka kwa shughuli za uchimbaji wa madini na uzalishaji wa mazao ya kilimo na bidhaa za viwandani” amesema.

Amesema, mwaka 2017 mfumuko wa bei kwenye eneo ulipungua na kufikia wastani wa 11.0%.

Amesema, mwaka 2016 mfumuko huo ulikuwa asilimia 11.3.

“Kushuka kwa mfumuko wa bei kwa nchi hizo kulichangiwa zaidi na kuimarika kwa sera za fedha na kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni pamoja na upatikanaji mzuri wa chakula uliotokana na hali nzuri ya hewa” amesema.

MKOA wa Rukwa umewasilisha Ofi si ya Rais, Tawala za ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi