loader
Picha

Rekodi mpya ya Ronaldo Kombe la Dunia yaandikwa

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameandika rekodi mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza kuifunga timu ya taifa ya Hispania mabao matatu (Hatrick).

Aidha mshambuliaji huyo ameibuka shujaa akiisaidia timu yake iliyotawaliwa na wakongwe kulazimisha sare ya mabao 3-3 dhidi ya timu ya Taifa ya Hispania. 

Mabao matatu ya Cristiano Ronaldo kwenye mchezo huo wa Kundi B wa fainali za Kombe la Dunia  yanaifanya timu hiyo ivune alama moja.

Ronaldo alianza kufungua akaunti yake ya mabao kwenye fainali za mwaka huu baada ya kupachika goli katika dakika ya nne tu ya mchezo kwa mkwaju wa penalti huku akirudi tena kwa kupachika mengine katika dakika za 44 na 88 kwa mipira wa adhabu.

Kwa upande wa  Hispania, mabao yalifungwa na Diego Costa dakika ya 24 na 55 huku jingine likifungwa katika dakika ya 58 na Nacho Fernandez.

Matokeo hayo yanaifanya Iran iendelee kushika nafasi ya kwanza katika Kundi B ikiwa na alama tatu baada ya kuifunga Morocco bao 1-0. Ureno inafuatia ikiwa na alama moja wakati nafasi ya tatu ikishikwa na Hispania ambayo pia ina alama moja, Morocco inashika mkia kwenye kundi hilo.

Kocha wa Juventus ya Italia, Max Allegri amesema, kama uamuzi ...

foto
Mwandishi: Lasteck Alfred

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi