loader
Picha

Kocha Argentina aomba radhi

KOCHA wa timu ya taifa ya Argentina, Jorge Sampaoli ameomba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo kufuatia kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Croatia na kuacha hewani matumaini ya Lionel Messi kufanya vizuri katika Kombe la Dunia.

Mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Ante Rebic – huku moja likitokana na makosa ya kipa wa Argentina Willy Caballero, yalifungwa na Luka Modric na Ivan Rakitic yaliihakikishia ushindi timu hiyo ya Ulaya na kuipeleka katika hatua ya timu 16 bora. Sampaoli alisema ni makosa yake na anaomba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo, ambao wamebaki wakitokwa na machozi kufuatia kipigo hicho kikubwa katika Uwanja wa Nizhny Novgorod. “Kwanza kabisa napenda kuomba radhi, hasa kwa mashabiki ambao wametoka umbali mrefu kuja kuiona Argentina,” alisema Sampaoli kwa upole.

“Kwa kweli nawajibika kwa matokeo haya lakini ilikuwa ndoto ya mashabiki kuwa timu yetu ingefika mbali, lakini haikuwa hivyo.” Kipigo hicho cha Kundi D kina maana kuwa Argentina, moja ya timu zilizokuwa zikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kabla ya kuanza kwa mashindano hayo na ambayo iliifungwa katika fainali mwaka 2014, iko hatarini kutolewa katika raundi ya kwanza ya mashindano hayo.

Hadi sasa ina pointi moja baada ya mechi mbili na sasa inatakiwa kuifunga Nigeria au Super Eagles katika mchezo wa mwisho ili kuweza kukwepa kuondolewa mapema. “Nilitakiwa kuangalia mipango kwa ajili ya mchezo huu,” alisema Sampaoli. Ikiwa mambo yamekwenda tofauti, mambo huenda yakawa mazuri huko mbeleni. Sifikirii kama ni haki kumtupia mzigo Caballero.” ‘ARI ILIMALIZIKA’ “Baada ya kutufunga tulivunjika moyo kabisa na hatukuweza kabisa kucheza soka letu na tulishindwa kubadili mwelekeo wa mchezo.”

Alisema timu pia ilishindwa kabisa kumlisha mipira zaidi Messi baada ya mipira mingi kupotea. Alipoulizwa kwanini alifanya mabadiliko mara tatu katika timu yake na kutumia mfumo wa 3-4-3, Sampaoli alisema kuwa alifikiri hiyo ilikuwa njia sahihi ya kuongeza shinikizo kwa Croatia. Lakini alikiri kuwa alifanya makosa. Croatia ilipata bao la kuongoza baada ya Caballero alipookoa mpira uliotua kwa Rebic, aliyepiga na kujaza wavuni katika dakika ya 53.

Nyota wa Real Madrid Modric baadaye naye alifunga katika dakika ya 80 kabla mchezaji mwenzake na Messi katika klabu ya Barcelona, Rakitic kufunga bao la tatu baada ya Croatia kuisambaratisha ngome ya Argentina katika muda wa majeruhi. Kipigo hicho kinaiacha Argentina ikikabiliwa na janga kama la mwaka 2002, wakati ilipotupwa nje ya mashindano katika hatua ya makundi baada ya awali kuonekana kama timu ambayo ingeweza kutwaa ubingwa wa Dunia.

Kocha wa Croatia, Zlatko Dalic alikiri kuwa alishangazwa kwa timu yake kuvuka baada ya mechi mbili lakini aliwaonya mashabiki wa timu hiyo kutobweteka, licha ya timu yao kufanya vizuri katika mashindano hayo hadi sasa. Lakini katika habari zingine mbaya kwa Argentina, kocha huyo wa Croatia alisema kuwa atawapumzisha baadhi ya wachezaji wake katika mchezo wa mwisho dhidi ya Iceland, wakati timu hiyo ya Amerika ya Kusini inataka Croatia kushinda. Naye mchezaji bora wa mchezo huo, Luka Modric alisema ushirikiano ndiyo kilikuwa kitu muhimu katika ushindi wao. “Juhudi za timu yetu (kilikuwa kitu muhimu) na hasa katika kipindi cha pili ambapo tulikuwa na umiliki mkubwa wa mchezo.

Kocha wa Juventus ya Italia, Max Allegri amesema, kama uamuzi ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi