loader
Picha

Simba Vs APR kazi ipo leo

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Simba, leo wanatupa tena karata yake ya pili kwenye michuano ya kombe la Kagame dhidi ya APR ya Rwanda kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ndio kinara wa kundi C ikiwa na pointi tatu ilizozipata katika mchezo wa kwanza dhidi ya Dakadaha ya Somalia, sawa na Singida United iliyo nafasi ya pili.

Simba ambayo ndio imelitwaa taji hilo mara nyingi, mara sita, inatarajiwa kuendelea kutumia sehemu ya wachezaji wapya iliowasajili kama ilivyokuwa kwenye mechi iliyopita.

Ingawa APR imekuwa na mabadiliko makubwa kwa kutokuwa na makali yake kama ilivyozoeleka kwenye michuano iliyopita ya ukanda huo, lakini hilo si sababu ya Simba kupata ushindi kirahisi kwani kwenye mpira lolote linawezekana.

APR ilipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Singida United katika mechi ya kwanza ya michuano hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Matokeo hayo ndiyo yatakayofanya mechi hiyo kuwa ngumu kwani APR bila shaka itahitaji ushindi leo ili kurudisha matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Baada ya mchezo wa leo, Simba itashuka tena uwanjani keshokutwa kukipiga dhidi ya Singida United, mechi nyingine yenye msisimko mkubwa kwenye kundi hilo kutokana na timu hizo kufahamiana vizuri maana zimeshakutana mara kadhaa kwenye michuano ya nyumbani.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza mapema kuweka ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi