loader
Picha

Yanga yamgeukia Kwizera

YANGA ipo mbioni kumalizana na kiungo Pierre Kwizera wa Rayon Sports ya Rwanda baada ya mazungumzo ya pande zote mbili kufi kia pazuri. Kiwango cha Kizwera ambaye ni raia wa Burundi kimemvutia kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, na kuutaka uongozi kuhakikisha wanamsajili ili afanye naye kazi msimu ujao.

Akizungumza na gazeti hili juzi Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika, alisema mazungumzo na nahodha huyo wa Rayon yanakwenda vizuri na kuna uwezekano mkubwa wakamalizana naye kabla ya michuano ya Kagame kumalizika. “Kocha amevutiwa na Kwizera na kazi ya kamati yangu ni kutekeleza agizo la kocha, nina imani siku chache zijazo tutafikia muafaka na Kwizera atavaa jezi za Yanga msimu ujao,” alisema Nyika.

Kiongozi huyo alisema Zahera ameanza kumfuatilia mchezaji huyo siku nyingi tangu walipocheza mechi ya hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika, hivyo mpaka kufikia sasa wameshajiridhisha kuwa ni mchezaji sahihi kwenye kikosi chake.

Kwa upande wake mchezaji huyo, alikiri kufuatwa na viongozi wa Yanga na kusema yupo tayari kutua timu hiyo endapo atapatiwa anachohitaji. Endapo dili hilo litafanikiwa itakuwa ni mara ya pili kwa Kwizera kucheza ligi ya Tanzania, mara ya kwanza ilikuwa misimu mitatu iliyopita ambapo aliichezea Simba lakini mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara hawakuridhishwa na huduma yake na kuamua kuachana nae.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza mapema kuweka ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi