loader
Picha

Simba, Singida mechi ya aina yake

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba na Singida United leo zinakutana katika mechi ya kukamilisha ratiba katika kundi lao kwenye michuano ya kombe la Kagame.

Timu hizo zinakamilisha ratiba kwani zote zimeshafuzu robo fainali baada ya kushinda mechi mbili mfululizo, ambapo zote zimefikisha pointi sita na Simba ikiongoza kwa uwiano mzuri wa mabao. Mechi ya leo itakayochezwa saa moja usiku kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, pamoja na kuwa ya kukamilisha ratiba lakini wapenzi wa soka wanatarajia kuona burudani safi kwa wawili hao hasa kutokana na matokeo yao ya kwenye Ligi Kuu msimu wa mwaka 2017/18.

Kwenye mechi za ligi, Simba imekuwa ikiitambia Singida mara zote mbili, ikiifunga mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa, kabla ya kuifunga 1-0 nyumbani kwao Namfua Singida. Mchezo mwingine utakaochezwa leo saa 10 jioni kwenye uwanja huohuo wa Azam utawakutanisha wenyeji Azam dhidi ya JKU. Azam imeshaingia robo fainali ikiwa na pointi sita hivyo kazi kubwa ipo kwa JKU yenye pointi nne inahitaji kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.

Mchezo mwingine ni Vipers ya Uganda itakayochuana dhidi ya Kator ya Sudan Kusini utakaochezwa saa 8 mchana kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo unaweza kuwa mgumu kwa timu zote mbili kwa vile hazina matokeo mazuri na kila mtu atapambana kumaliza na pointi angalau kupata nafasi ya kucheza robo fainali kama ‘best looser’ Pia, APR ya Rwanda itachuana na Dakadaha ya Somalia utakaochezwa saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa. Wote wanahitaji pointi ili angalao nao wawemo kwenye ‘kapu’ la ‘best looser’.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza mapema kuweka ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi