loader
Picha

Kagere- Simba wamenipa fedha za kutosha

MFUNGAJI wa bao la ushindi la Simba katika mchezo dhidi ya APR Meddie Kagere amesema hakuona sababu ya kuendelea kubaki na Gor Mahia kwa kuwa Simba SC walimuwekea fedha za kutosha.

Wiki moja iliyopita Simba ilikamilisha usajili wa mkali huyo kutoka Rwanda kwa dau linalodaiwa kuwa Sh milioni 120 na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Kagere amesema, mkataba wake na Gor Mahia ulikwisha hivyo wakati anasubiri kuwekwa chini kuzungumzia mkataba mpya Simba ilimwahi kwa dau alilotaja kuwa asingeweza kukataa.

Amesema, siku zote akiwa kama mchezaji anatakiwa kupendwa na viongozi na mashabiki, pamoja na hilo pia huwa anaangalia sehemu yenye maslahi kutokana na kuwa soka ndiyo kazi yake.

“Kwa sasa sina timu yoyote, nipo Simba tu, Gor Mahia sikuwa na mkataba nao walikawia kuniongelesha, Simba walikuwa wananipenda zaidi ndo wakaniwahi, sasa kama mtu anakupa kitu kizuri kwa nini usiende,” amesema Kagere.

Pamoja na upana na ubora wa wachezaji wa Simba, Kagere amesema yupo tayari kukabiliana na changamoto zote ikiwemo ushindani wa namba na kusisitiza kama huwezi kuchuana pia huwezi kucheza mpira.

Kagere alizungumzia bao lake la kwanza la penalti alilofunga juzi kwenye michuano ya Kagame na kusema kuwa huo ni mwanzo, mengi zaidi yanakuja kikubwa ni kuendelea kushirikiana na wachezaji waliopo ili kufika lengo na klabu yao.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza mapema kuweka ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi