loader
Picha

Simba, Gor Mahia muziki mnene leo

MABINGWA wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Simba leo wanakutana na AS Ports ya Djibout katika mchezo wa robo fainali Kombe la Kagame utakaochezwa kwe nye uwanja wa Taifa. Mchezo huo utachezwa saa 1.00 usiku.

Simba haijapoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa michuano hiyo, ambapo kati ya michezo mitatu, imeshinda miwili na kupata sare moja. Kikosi cha wekundu hao kinachoongozwa na Kaimu Kocha Mkuu Masoud Djuma kina wachezaji wengi wapya na wale waliokuwa msimu uliopita waliokosa nafasi ya kucheza wakitumia michuano hiyo kuwatathmini.

Tayari baadhi wamekuwa ni moto na huenda wakawa mwiba katika mchezo wa leo kama vile Meddie Kagere aliyecheza mechi mbili na kufunga mawili, Marcel Kaheza aliyefunga bao moja na Adam Salamba mwenye mabao mawili. Wapinzani wao Ports ya Djibout walicheza michezo mitatu na kati ya hiyo walishinda mmoja, sare moja na kupoteza mmoja. Wanaweza kutazamwa kama vibonde kwa kuwa walipita kama washindwa bora lakini sio timu ya kubeza na katika michezo yote walicheza vizuri na kuonesha ushindani.

Aidha, Gor Mahia itachuana na Vipers ya Uganda katika mchezo utakaochezwa saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hiyo ya Kenya haijapoteza mchezo wowote katika mitatu waliyocheza, wameshinda mmoja na kupata sare mbili. Na wapinzani wao wameshinda mchezo mmoja, sare moja na kupoteza mmoja.

Wote ni wazuri na yeyote anaweza kupata matokeo inategemea na walivyojiandaa. Mechi nyingine zitachezwa kesho wakati mabingwa watetezi Azam FC wakitarajiwa kuchuana na Rayon Sports ya Rwanda saa 10 jioni na Singida United dhidi ya JKU ya Zanzibar saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Taifa. Mshindi kati ya Simba na Ports atacheza na mshindi kati ya Singida na JKU kwenye hatua ya nusu fainali. Na mshindi kati ya Gor Mahia na Vipers atacheza na mshindi kati ya Azam na Rayon.

KOCHA wa Y anga, Mwinyi Zahera ameahidi kuendeleza ushindi katika ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi