loader
Picha

Gesi asilia majumbani kwa bei nafuu

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imeipa kampuni yake tanzu ya gesi Tanzania (GASCO), kazi ya kusambaza gesi asilia majumbani na kuhakikisha inawafikia wananchi kwa bei nafuu.

Kampuni hiyo inayofanya uendeshaji, matengenezo ya miundombinu yote ya gesi asilia ya serikali nchini, sasa itasambaza miundombinu kwa wateja wa majumbani kwa kasi na gharama nafuu.

Kaimu Meneja Mkuu wa GASCO, Baltazar Mrosso akizungumza katika banda la TPDC katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DIFT) alisema katika usambazaji huo, miradi mingine mikubwa itatekelezwa kwa kutangaza zabuni.

Alisema kuanzia Juni mwaka huu, kampuni hiyo ilisajiliwa na Bodi ya Usajili Wakandarasi na kupewa jukumu hilo la kuwaunganishia wateja majumbani kwa lengo la kupunguza gharama za kuunganishwa na kupunguza mlolongo wa kumpata mkandarasi TPDC iliamua kutumia kampuni yake tanzu.

“Sasa TPDC inachofanya ni kutafuta wateja kisha kutuachia sisi tunatengezeza, kuendesha na kujenga miundombinu yote mpaka kwa mteja kisha kuendelea kufanyia ukarabati wa mara kwa mara kuhakikisha gesi inafika kwa usalama,” alisema.

Mrosso amesema wanaanza na nyumba 38 mpya katika maeneo ya Mikocheni, kisha Mlalakua huku wakiendelea na kuangalia maeneo ya Sinza wanakotarajia kupeleka miundombinu hiyo katika nyumba 100 pamoja na maeneo mengine ambayo miundombinu iko vema.

Mhandisi wa TPDC, Limi Lagu amesema hadi kufikia Juni mwakani, watakuwa wameshasambaza gesi ya majumbani kwa wateja 1850 wa mkoa wa Dar es Salaam na Mtwara.

Alisema mpaka sasa nyumba 38 za Mikocheni zimefikiwa na mradi huo huku wakiendelea kuwafungia wateja wengine 1,000 wanaotoka maeneo ya Mwenge, Ubungo, Sinza, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Tegeta.

Limi amesema pia wamelenga kuwaunganishia wateja 850 wa Mkoa wa Mtwara na Lindi, ambao ni awamu hii ya kwanza wananufaika na gesi hii baada ya mifumo ya gesi kupita maeneo yao, ambapo kwa kushirikiana pia na uongozi wa serikali ya mitaa kuwapa elimu juu ya umuhimu wa matumizi ya gesi asilia.

Amesema pia TPDC inao mradi wa usambazaji gesi mikoani kwa kushirikiana na kampuni binafsi, ambapo tayari mchakato wa awali umeanza.

Ametaja mikoa itakayofikiwa na mradi huo ni Tanga, Pwani, Dodoma na Dar es Salaam na tayari wameandika dokezo kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Nishati.

MKUU wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi amekataa ombi la ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi