loader
Picha

Tembo kuipamba Dodoma

PICHA ya mnyama tembo itawekwa kwenye mizunguko ya barabara jijini Dodoma kwa ajili ya kutangaza asili ya jina la jiji hilo.

Wakati wa kutia saini kati ya Jiji la Dodoma na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema picha ya mnyama tembo ni muhimu kuwepo katika mizunguko hiyo.

Amesema picha ya mnyama tembo ni muhimu kuwepo katika mizunguko ya barabara ya Singida, Arusha na Dar es Salaam kutokana na ukweli kwamba mnyama huyo alizama katika eneo la jiji hilo ndipo wenyeji wakapaita idodomya, yaani imezama.

Kunambi amesema pia kuna mazungumzo yanaendelea na Mamlaka ya Maji na Usafiri wa Mazingira Dodoma (Duwasa) kwa ajili ya kuhakikisha eneo ambalo mnyama huyo alizama linawekewa kumbukumbu maalumu.

Amesema katika kuenzi jina la Dodoma, eneo ambako alizama mnyama huo karibu na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi litaenziwa na kuwekewa alama maalumu ya kumbukumbu.

Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Joyce Msuyu aamesema, wao wameamua kulipamba jiji la Dodoma hivyo wapo tayari kulipamba kadiri ya mapendekezo ya viongozi wa mji hilo.

Amesema wapo tayari kupamba picha ya mnyama tembo katika mizunguko hiyo kwa sababu kwanza ni kutangaza utalii wa nchi lakini pia ni kutangaza jina la asili ya jiji hilo.

Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe, amesema ni fursa adhimu kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuamua kushirikiana katika kuipamba Dodoma.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, imetia saini na Jiji la Dodoma kwa ajili ya kuweka mapambo mbalimbali katika mizunguko mitatu katika barabara ya Arusha, Singida na Dar es Salaam kuanzia mwezi huu.

MKUU wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi amekataa ombi la ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi