loader
Picha

Waziri aagiza Nyuki wawakabili tembo

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amesema kuanzia sasa nyuki watatumika kukabili uvamizi wa tembo wanaoharibu mazao shambani na kusababisha vifo wilayani Kalambo mkoani Rukwa.

Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara, Gaudence Milanzi kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kuhakikisha vinaundwa vikundi.

Vikundi hivyo vitawezeshwa mizinga ya kisasa itakayopangwa katika mipaka ya vijiji vinavyozunguka hifadhi ya msitu wa Mto Kalambo na pori la akiba la Lwafi kukabiliana na tembo hao.

Amezitaka taasisi za uhifadhi za Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa) na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kusaidia kuunda vikundi hivyo kwa kushirikiana na wilaya ya Kalambo.

Ametoa agizo hilo baada ya kupokewa na mabango katika kijiji cha Kisumba, Kata ya Kasanga akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Kalambo ambapo wananchi walizuia msafara wake na kumueleza kero zao.

Mkazi wa Kijiji cha Kisumba, Imelda Donizi amemweleza waziri Kigwangalla kuwa tembo wamekuwa kero kwa kuwa wameharibu mazao yao shambani na kutishia usalama wao kwamba wana wasiwasi kuwa wasipodhibitiwa watasababisha uhaba wa chakula.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Julieth Binyura amemweleza waziri kuwa makundi ya tembo yamevamia mashamba 66 na kuharibu mazao ya chakula katika kata za Kisumba, Mkowe na Mpombwe.

"Mkifuga nyuki kwa kupanga mizinga ya kisasa katika mipaka ya vijiji vinavyozunguka pori la akiba la Lwafi na hifadhi ya msitu wa Moto Kalambo tembo hawatawavamia tena kwa kuwa harufu ya nyuki itawakimbiza pia ufugaji huo wa nyuki utawaongezea kipato na mtaachana na ukataji miti kwa ajili ya mkaa," amesema Dk Kigwangalla.

MKUU wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi amekataa ombi la ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Kalambo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi