loader
Picha

NEC yampongeza JPM, yamteua Chiza

Kikao cha Kamati Kuu maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Christopher Chiza mgombea ubunge jimbo la Buyungu.

Kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi ndogo ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam pia kimempongeza Rais John Magufuli kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya chama hicho na kasi kubwa ya kupeleka maendeleo na huduma za kijamii hasa maeneo ya pembezoni na mijini.

Taarifa ya Katibu wa NEC Itikadi na uenezi, Humphrey Polepole imeeleza kuwa, kikao hicho kimepokea na kupongeza taarifa ya kuwasili kwa ndege kubwa ya Serikali, mpya nay a kisasa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner itakayokodishwa kwa Shirika la Ndege la Taifa (ATCL).

Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. John Magufuli.

MKUU wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi amekataa ombi la ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi