loader
Picha

Elisante Ole Gabriel ainadi Tanzania Marekani

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biadhara na Uwekezaji, Profesa Elisante ole Gabriel ameongoza ujumbe wa Watanzania katika Mkutano wa Mpango wa Uuzaji wa Bidhaa za Afrika katika Soko la Marekani pasipo Kutozwa Kodi (AGOA) unaofanyika jijini Washington, Marekani.

Agoa ilianzishwa na aliyekuwa Rais wa Marekani, Bill Clinton mwaka 2000 ambapo ukomo wake ni mwaka 2025. Akiwa nchini Marekani, Katibu Mkuu, Ole Gabriel ameshiriki kikao cha Makatibu Wakuu wanaohusika na sekta za biashara kwenye nchi zao. Jana kilifanyika kikao cha ngazi ya mawaziri wenye dhamana ya biashara.

Akizungumzia mkutano huo, Profesa Ole Gabriel alibainisha kuwa mkutano huo utawahusisha mawaziri, makatibu wakuu, wataalamu pamoja na mabalozi wa Afrika ili kujadiliana kuhusu masuala ya kibiashara na wenzao wa Marekani. Mkutano huo utazungumzia pia udumishaji wa ushirikiano wa biashara kati ya Marekani na Afrika.

“Utafanya pia tathmini ya mafanikio yaliyopatikana, ikiwa ni pamoja na kujadiliana undani wa namna ya kutatua changamoto zake,” alisema Katibu Mkuu huyo. Kwa mujibu wa Profesa Elisante, mpango huo unafikia ukomo mwaka 2025 na kwamba mkutano huo utajadili mustakabali wa mahusiano ya kibiashara utakavyokuwa kati ya Afrika na Marekani baada ya kumalizika kwa kipindi cha ushirikiano mwaka 2025. “Mkutano huu unafanyika katika kipindi mwafaka ambapo Tanzania inaendelea na harakati za kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda, ni mkutano muhimu kwetu kama nchi na unaendana na azma yetu ya kukuza uchumi. “Unafanyikia katika Ukumbi wa Benki ya Dunia, Washington DC na ujumbe ninaouongoza umepokewa vizuri na Balozi wetu hapa, Wilson Massilingi, ” alisema Profesa Ole Gabriel.

MKUU wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi amekataa ombi la ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi