loader
Picha

Wageni 8 mbaroni Dodoma

IDARA ya Uhamiaji mkoani Dodoma imewakamata na kuwashikilia raia wanane wa kigeni kwa makosa ya kuwepo nchini kinyume cha sheria.

Pia idara hiyo ya Uhamiaji inawashikilia watanzania wawili kwa makosa ya kutotoa ushirikiano wakati askari walipokuwa wakitaka kufanya upekuzi.

Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dodoma, Peter Kundy amewaeleza waandishi wa habari kuwa, raia hao walikamatwa katika vizuizi vya barabarani wakati wa doria.

Wengine walikamatwa katika msako ulioendeshwa na idara hiyo ya uhamiaji jijini hapa.

Kundy aliwataja watu waliokamatwa kuwa ni Emmanuel Ayala, Deginat Aseta (25), Delamo Lenjamo (24), Samweli Eyasu (27) na Tawala Ababa (24) wote wa Ethiopia.

Wengine ni Sada Niyonkulu (38) (Burundi), Amuri Hererimana (44),(Rwanda) na Akena Thomas.

Kundy amesema, Watanzania waliokamatwa kwa kutotoa ushirikiano kwa askari wa upekuzi ni pamoja na Kahlidi Kimbe (40) na Shineni Mwindandi.

Ofisa huyo wa Uhamiaji alisema idara hiyo itaendelea kutoa elimu ya uraia kwa wananchi wote na kuwaomba kutoa taarifa za wahamiaji haramu na watu wanaotiliwa mashaka.

“Wananchi watupatie taarifa mbalimbali kwa kupitia namba ya simu 0746118086 ambayo ipo hewani muda wote,” alisema. Ofisa uhamiaji huyo alisema misako na doria itaimarishwa katika maeneo yote muhimu.

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi