loader
Picha

Abiria wote wa ndege kukaguliwa

ABIRIA yeyote bila kujali cheo chake anatakiwa kukaguliwa kwenye viwanja vya ndege nchini kwa usalama wa nchi na usalama wake.

Akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari jijini hapa, Mkaguzi Mwandamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga (TCAA), Salim Msangi amesema, kila mtu anatakiwa kukaguliwa bila kujali cheo chake.

Msangi amesema, kwa kuzingatia mkataba wa Vienna wa mwaka 2006, kila abiria anatakiwa kukaguliwa bila kujali cheo chake au madaraka aliyonayo wakati anapoingia viwanja vya ndege.

Amesema kila abiria anatakiwa kuhakikisha anakaguliwa kwa ajili ya kuepusha matatizo mengi ambayo yanaweza kujitokeza katika usafiri wa anga.

"Hata kama mashine zinakuwa zimeharibika, wakaguzi wanatakiwa kutumia mikono kukagua kwa kuzingatia jinsia wa kike akaguliwe na wa kike," alisema. Kaulimbiu inasema,

"Hatutakiwi kukataa kukaguliwa, bali tuhoji ni kwa nini hatukaguliwi, kutokana na umuhimu wa kukaguliwa hasa kwa mazingira ya sasa".

Amesema hata wageni au wamiliki wa ndege wanaotaka kutumia viwanja vya ndege nchini wanatakiwa kuleta mpango wa usalama wa uendeshaji ndege wao ambao unatakiwa uendane na sheria za Tanzania.

Amesema sheria ya nchi iliyopo ya mwaka 2017, inayofanyiwa marekebisho inataka kufanya ukaguzi kwa wasafiri na wafanyakazi lakini pia kuwalinda watu wanaofika kuwapokea ndugu zao.

Lakini pia mkaguzi lazima awe amepata mafunzo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, akifeli kufanya ukaguzi au kubaini kitu basi anapokwa leseni.

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) la Umoja wa Mataifa (UN) ambalo Tanzania ni mwanachama na imeridhia, kila nchi inatakiwa kuwa na ukaguzi wa usalama wa anga na abiria wanaosindikiza.

Meneja wa TCAA Dodoma, Ludovic Ndumbaro amesema wakati anafungua mafunzo hayo kuwa, sekta ya usafiri wa anga na sekta ya usifirishaji kwa ujumla vina mchango muhimu katika kukuza uchumi wa nchi.

Mchango huo ni pamoja na kukuza usafiri huu kwa muhimili muhimu wa utalii hasa ikizingatiwa asilimia kubwa ya watalii ambao wanaotoka nchi za magharibi na mashariki ya mbali wanategemea usafiri wa anga.

Serikali imeagiza viongozi wa Mamlaka ya Usafirishaji Nchi Kavu na ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi