loader
Picha

Watumishi wanaoichafua TRA kukiona

WAZIRI wa Fedha na Mpango, Dk Phillip Mpango amesema ni bora Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ibaki na watu wachache waadilifu kuliko kubaki na wanaoipaka tope.

Mpango amewataka watumishi kuishi kwa maadili na kuepuka kifo cha aibu cha kuitwa mwizi wa kodi na watambue sifa itakayoachwa duniani.

Waziri Mpango alisema hayo baada ya kufika katika banda la TRA lililoko katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) yanayotarajiwa kumalizika kesho katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

“Changamoto yangu kubwa ni kuhitaji kazi ya ziada, ni heri nibakie na watumishi wachache waadilifu ili wadai kodi ambayo ni halali," alisema Mpango na kuongeza kuwa wapo watumishi wanaoipaka matope TRA.

Akiwa kwenye kitengo cha maadili alihoji watumishi waliofukuzwa kazi kutokana na kutokuwa na maadili mazuri kwa mwaka 2017/18 na kujibiwa kuwa ni wanane. Alitaka kufahamu kama wafanyakazi hao walifukuzwa kazi pekee au kulikuwa na hatua nyingine zilizochukuliwa.

"Msinichekee kwani huwezi kujifunika blanketi moja na nyoka ni bora kutafuta Watanzania wenye maadili ili kufanya nao kazi, mngeondoa wengi msingelalamikiwa hivyo na Watanzania, maadili yanaumiza kila siku, Kamishna na wakubwa wote waambiwe," alisema.

Katika kitengo cha mapato aliiagiza TRA kutafuta mazuri yaliyofanywa na serikali kupitia fedha za wananchi ili waweze kuona na kulinganisha makusanyo ya kodi na miradi mbalimbali ya maendeleo kwani kuweka namba katika kuta za maonesho hayo haisaidiii.

Katika kitengo cha kodi ya majengo alisema ipo haja ya kuanza mapema kuelimisha kuhusu kodi hiyo. Katika kitengo cha mashine ya kielektroniki (EFDs) alisisitiza kodi kukusanywa vizuri huku TRA wakitakiwa kufanya ukaguzi kwa kuwa serikali imekuwa ikiibiwa kizembe.

"Bunge limeisha, zamu hii siwachekei anayehusika na ukaguzi mtaa fulani ninaye, anayewabugudhi walipa kodi pia ninaye," amesema na kuwaasa kuacha kuzoeana na wafanyabiashara.

Serikali imeagiza viongozi wa Mamlaka ya Usafirishaji Nchi Kavu na ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi