loader
Picha

'Bila kuvaa helmet pikipiki haiwaki'

ALIYEKUWA Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga ameshauri teknolojia zinazobuniwa na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA) ziongezewe utaalamu ili kuifikia sehemu kubwa ya jamii, hasa mfumo wa pikipiki kutowaka mpaka dereva avae kofia.

Mpinga amesema hayo alipotembelea banda la VETA na kujionea teknolojia zilizobuniwa na wanafunzi mbalimbali wa vyuo, hivyo kwa kushirikiana na walimu.

Amesema, katika zama za kuelekea uchumi wa viwanda ni vyema jamii kubwa nchini ikashirikishwa ili teknolojia hizo mpya zienee kwa kasi hasa katika maeneo ya vijijini.

Amesema, kuna mashine ya kukausha mazao, mfumo wa kuzima taa hata kama upo mkoa au nchi nyingine pamoja na hiyo ya kuwasha bodaboda kwa kutumia kofia ya abiria na dereva.

Mpinga amewapongeza Veta kwa kubuni mifumo ya kisasa yenye gharama nafuu itakayosaidia kuikomboa jamii kiteknolojia.

Mwanafunzi Rentius Pesha amesema mfumo huo huzuia ajali za kizembe na wizi na kuomba serikali kutunga sheria ya kutaka pikipiki zote kwenda Veta kufungwa mfumo huo utakaosaidia kukabiliana na athari kichwani ajali zinapotokea.

Pikipiki hiyo iliyopo katika viwanja ya Maonesho ya 42 ya Biashara, imewekwa kifaa maalumu kwenye kofia za pikipiki na kama dereva au abiria hatavaa helmet pikipiki haitawaka.

Amesema, lengo la kubuni mfumo huo ni kubainisha teknolojia siyo lazima itoke nje ya nchi, bali VETA ina uwezo wa kuvumbua teknolojia kuokoa nguvukazi ya taifa kwa kuokoa madereva.

Serikali imeagiza viongozi wa Mamlaka ya Usafirishaji Nchi Kavu na ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi