loader
Picha

ATCL kimataifa zaidi

Mkurugenzi Mkuu wa ATCl, Ladislaus Matindi amesema wamejipanga vizuri ili kujitanua kibiashara na kurudi katika mfumo wa kimataifa wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Ndege (IATA).

Amesema ATCL iliondolewa katika mfumo wa kimataifa wa utoaji wa huduma na ununuzi wa tiketi kwa kukabiliwa na madeni makubwa.

Kwa mujibu wa Matindi, madeni ambayo yaliitia hasara kubwa ATCL yalitokana na udanganyifu wa mikataba ya huduma, manunuzi na ukodishwaji wa ndege.

Amesema kitendo cha kutia saini na kampuni hiyo maana yake sasa ATCL itarudi tena katika utoaji wa huduma zake mbalimbali kwa kutumia mgongo wa kampuni hiyo inayoheshimika duniani.

Matindi amesema, taratibu zote zimefuatwa katika makubaliano na watoaji wa huduma za ndege za kimataifa Hahn Air, ikiwemo kupata baraka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuridhia.

Awali Makamu wa Rais wa kampuni hiyo, Steve Krackstedt amesema, wameingia mkataba na ATCL baada ya kuridhishwa na juhudi zake kujiimarisha ili kurudi mfumo wa kibiashara.

Amesema kazi kubwa imefanywa na ATCL kuimarisha huduma zake ikiwemo kununua ndege mpya kwa ajili ya safari zake nchini na nje ya nchi ikionesha utayari kufanya biashara.

BAADHI ya wafugaji wilayani Rungwe wameitaka Kampuni ya Asas inayojihusisha ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi