loader
Picha

Kauli ya RC Tabora inafaa

Kutokana na umuhimu wa zao hilo, tunaunga mkono kauli iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, ambapo kwanza aliwahimiza wananchi kulima pamba kwa wingi.

Alisema hayo jana kwa nyakati tofauti, alipozungumza na wakulima wa pamba wa vijiji vya Mondo, Buchenjegele na Mwashiku Kata ya Mwashiku wilayani Igunga.

Alikuwa katika wilaya hiyo kukagua maendeleo ya kilimo cha pamba. Mwanri anasema wananchi wanatakiwa kuongeza maradufu uzalishaji wa pamba, hasa wakati huu ambapo azma ya serikali ni kufikia uchumi wa viwanda.

Anasema baadhi ya viwanda vitakavyoanzishwa katika maeneo mbalimbali nchini, vitahitaji pamba ya kutosha, hivyo upo umuhimu mkubwa wa kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Pili, tunaunga mkono kauli ya Mwanri ya kuwataka wakazi wa Tabora, kutumia fedha zinazotokana na pamba, kuboresha barabara, hospitali, shule, zahanati na makazi. Mwanri anasema ni aibu kwa kiongozi kama yeye, kuona wananchi wake wanahangaika na maisha, ilihali wana uwekezaji mkubwa wa zao la pamba.

Anaeleza kuwa ni vyema wananchi watumie zao la pamba, kubadilisha maisha yao. Mkuu huyo wa Mkoa anasema anatamani siku atakayoondoka Tabora, wananchi wakumbuke kuwa alikuwepo mkuu wa mkoa ambaye aliwafanya wapate maisha kutokana na zao la pamba.

Anasisitiza kamwe hatakubali kuwa mkuu wa mkoa ambaye wananchi wake ni masikini, vinginevyo hana sababu ya kupelekwa Tabora na Rais John Magufuli.

Wananchi na viongozi wa ngazi mbalimbali nchini, hawana budi kuunga mkono msimamo wa mkuu huyo wa mkoa, ambaye amedhamiria kuleta mapinduzi katika kilimo cha pamba.

Ni dhahiri kuwa Mwanri amelazimika kutoa kauli hiyo kutokana na kilimo cha zao hilo, kushindwa kuleta mabadiliko katika maisha ya wananchi. Ni lazima kuanzia sasa kilimo cha zao hilo, kiboreshe maisha ya wakulima.

Hakuna sababu ya kuendelea kuwa maskini wakati pamba inalimwa kwa wingi.

KUMEKUWA na ukiukwaji wa sheria na kanuni zake kwa madereva ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi