loader
Picha

KQ yajizatiti kupunguza hasara

Alisema kuanzishwa safari mpya katika Bara la Afrika na Marekani, na kuimarika kwa hali ya kisiasa, kunachangia kampuni hiyo kupata faida zaidi ya hasara.

Kwa mujibu wa mtendaji huyo, KQ ilipata hasara ya Dola milioni 61 katika kipindi cha miezi tisa iliyopita tangu Aprili hadi Desemba 2017.

“Hasara hiyo imesababishwa na mambo mbalimbali kama vile mapungufu ya wakurugenzi wetu, kutotulia kwa baadhi ya nchi za Kiafrika na kuwepo kwa chaguzi mbili za Kenya mwaka jana,” amesema Sebastian Mikosz.

Mikosz ametaja sababu nyingine za kampuni kupata hasara hiyo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa bei ya mafuta kwa asilimia 14.

Amesema, kuongezeka kwa bei ya mafuta ni changamoto kubwa katika kutafuta faida, hivyo kampuni kuishia kupata hasara na kupunguza kasi ya uendeshaji wa kampuni.

“Hali ya kisiasa nchini imetulia na kutuhakikishia biashara yetu kuendelea vizuri baada ya Rais Uhuru Kenyatta kukutana na kufanya mazungumzo na Raila Odinga Machi 9 mwaka huu hatua ambayo tunaamini itaimarisha uchumi wa nchi,” amesema Mikosz.

Kutokana na hali hiyo, Mikosz alisema anaamini mwaka 2018 utakuwa mzuri kwa KQ kwa kuwa mwezi Oktoba 2018 safari za moja kwa moja kwenda New York na Mauritius na safari zingine za moja kwa moja kwenda Cape Town, Afrika Kusini zitaanza.

Mikosz amekiri kuwa si rahisi faida kuonekana ndani ya mwaka huu. “Hali nzuri ya kifedha itaanza kuonekana mwaka 2019 kutokana na ongezeko la mapato hadi asilimia 10 kwa safari za Nairobi hadi New York pekee,” aliongeza Mikosz.

UTALII unachangia asilimia 25 ya pato la ndani Zanzibar na ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi