loader
Picha

Ni aibu RT kutopeleka wanariadha Algeria, Hispania

Mbali na mbio hizo za nyika, pia Tanzania hatukupeleka wanariadha katika mashindano ya dunia ya mbio za nusu marathon, ambazo zinafanyika leo huko Valencia, Hispania.

Riadha Tanzania kwa muda mrefu waliahidi kupeleka wachezaji katika mbio hizo za dunia za nusu marathon na waliwaandaa wanariadha wawili, Jackline Sakilu na Ezekiel Ngimba lakini wameshindwa kwenda Hispania baada ya kutopewa ruhusa na mwajiri wao, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kwa kweli ni aibu kwa Tanzania kushindwa kupeleka wanariadha katika mashindano makubwa, na wakati mwingine ni kutokana na uzembe tu wa viongozi wa riadha.

RT, wenyewe wanadai kuwa walifanya taratibu zote za kuwaombea ruhusa wanariadha hao, lakini mimi nahofu kuwa huenda maombi hayo yalichelewa kufika kwa JWTZ na ndiyo maana wakanyimwa ruhusa.

Jeshi na waajiri wengine huwa na taratibu zao na siyo rahisi hasa kwa taasisi kama ya jeshi kukurupuka na kutoa ruhusa kirahisi muda mfupi kabla ya safari.

Viongozi wa RT mnatakiwa mjifunze kutoka kwa akina Juma Ikangaa na Filbert Bayi, ambao walikuwa askari wa JWTZ na wakati wote walikuwa wanariadha wanaoshiriki mashindano ya mara kwa mara nje ya nchi.

Ikangaa baada ya kustaafu mbio aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa RT, hivyo atakuwa anajua taratibu alizokuwa akizitumia kuwaombea ruhusa wanariadha wa Jeshi, hivyo RT waombe ushauri wake.

Mbio za dunia za nusu marathon zina zawadi nono, hivyo tumewakosesha wanariadha wetu kupata zawadi hizo kwa kushindwa kuwapeleka.

Mbali na zawadi pia mbio hizo zingewezesha wachezaji wetu kupata uzoefu wa mashindano ya kimataifa na kuwafanya kuyazoea mashindano hayo na kuwawezesha kufanya vizuri katika mbio mbalimbali.

Zawadi katika mbio hizo hutolewa kwa timu pamoja na kwa mshindi wa wanariadha mmoja mmoja aliyefanya vizuri katika mbio zake.

RT tujitafakari na kuhusu kushindwa kupeleka wanariadha au timu katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na badala yake tuwe nakini na ratiba za kimataifa.

UAMUZI wa serikali wa kuwasamehe wafanyabiashara na walipakodi riba na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi