loader
Picha

Ujenzi viwanda kila mkoa asilimia 49

Takwimu hizo zimepatikana baada ya wakuu wa mikoa 26 kuelezea hatua waliyofikia katika utekelezaji wa agizo hilo lililolenga kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli la kupeleka nchi katika uchumi wa viwanda.

Akizungumza katika kikao kazi cha kupitia bajeti ya Ofisi ya Rais (Tamisemi) na mikoa ambacho kilifuatana na upokeaji wa taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo, Jafo alisema hadi sasa vimejengwa viwanda 1,285 kati ya 2,600 ambavyo vinatarajiwa kujengwa ndani ya mwaka mmoja ambayo ni sawa na asilimia 49.4.

Alisema agizo hilo bado linaendelea kutekelezwa ambapo hadi kufikia Desemba 31, mwaka huu kila mkoa unatakiwa kuwa na viwanda 100.

“Viwanda hivi vilivyojengwa vina mchanganyiko mbalimbali ikiwemo viwanda vikubwa, vya kati na vidogo, mna mikakati mikubwa ambayo itawezesha kuwa na mchanganyiko wa viwanda vikubwa na vidogo,” amesema Jafo.

Alibainisha kuwa kupitia wakuu wa mikoa ajenda ya Rais Magufuli ya viwanda inatekeleza na kuwataka waendelee kutekeleza. "Wakati tunapiga hatua katika suala la viwanda, lakini wapo wengine ambao wanataka kuona kuwa tumefeli, na wengine wanaotaka kubainisha kuwa ajenda ya Rais ya viwanda haitekelezeki, lakini kwa hatua hii tumebainisha kuwa inatekelezeka," amesema.

Awali, kila mkuu wa mkoa alibainisha hatua aliyofikia. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akibainisha mkoa wake kuwa na viwanda 88 vipya vilivyojengwa.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema katika mkoa huo wamejenga viwanda 22 ambavyo ni vikubwa na vya kati na vingine vipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alisema zimetengwa hekari 307,595 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na hadi sasa tangu kutolewa kwa agizo la Waziri Jafo vimejengwa viwanda 45 vipya ambavyo vimetoa ajira mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema mkoa huo unaendelea kutekeleza mkakati wake wa bidhaa moja kwa wilaya moja na kwamba tangu agizo hilo viwanda mbalimbali 18 vipya vimejengwa.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema viwanda vipya vilivyojengwa ndani ya agizo hilo ni 124 huku Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack akisema kwake amejenga viwanda 126.

Aidha, asilimia kubwa ya wakuu wa mikoa walibainisha baadhi ya changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa agizo hilo kuwa ni kukosekana kwa umeme, maji, masoko, ukubwa wa bei ya aridhi na ardhi kubwa kutopimwa.

UTALII unachangia asilimia 25 ya pato la ndani Zanzibar na ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi