loader
Picha

ZIPA yahamasisha uwekezaji wa ndani

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Salum Khamis Nassor alisema Watanzania wakiwemo Wazanzibari wanaotaka kuwekeza waitumie mamlaka hiyo kwa kuwa haikuanzishwa kwa ajili ya watu kutoka nje ya nchi tu.

Alisema mjini Unguja kuwa, fursa wanazopata wageni zipo pia kwa ajili ya Watanzania hivyo wanaweza kuitumia ZIPA ili wapate maendeleo na kuchangia kukuza uchumi wa nchi yao.

“Kwa hiyo nitoe mwito huo kwa wawekezaji wenye uwezo, wa ndani kuwa mbele kuliko hata hawa wageni. Kwa hiyo sisi tumefanya kwa makusudi kwamba, tunatoa preference (kipaumbele) kwa wawekezaji wa ndani zaidi kuliko wageni. Zile fursa zote wanazosikia wageni wanazipata nazo zipo kwa ajili yao na pengine zipo za ziada kuliko hata wale wageni,”alisema Nassor.

Alisema, ZIPA ipo kwa ajili ya wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi hivyo wakiitumia mamlaka hiyo pia serikali itanufaika kutokana na uwekezaji wa mitaji.

“Mara nyingi mamlaka hii inatumika kuidhinisha mambo ambayo yanawezesha watu sasa kuaminiwa kupata mitaji kwa ajili ya kuja kuwekeza katika nchi yetu. Sasa hii isiende kwa wageni kwa asilimia 100 na wenyeji nao wanayo fursa hiyo,” alisema.

Alitoa mfano kuwa, viwanda vingi vya maji Zanzibar ni wananchi wa visiwani humo, na kwamba, waliitumia ZIPA kupata mitaji waliyoitumia kuwekeza.

Kwa mujibu wa Nassor, mamlaka hiyo ilianzishwa kwa sheria namba 11 ya mwaka 2004 ili iishauri serikali kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji kutoka kwa wafanyabiashara wa ndani na nje.

Kwa mujibu wa Nassor, mamlaka hiyo ina majukumu makubwa matatu na kwamba, sheria iliyoianzisha inaitaka ikuze na ilinde mitaji ya watu binafsi, ikuze na iwezeshe biashara ya ndani na nje, na isimamie maendeleo ya miundombinu katika maeneo huru ya biashara.

UTALII unachangia asilimia 25 ya pato la ndani Zanzibar na ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi