Neymar aumia tena

DARWIN Nunez na Nicolas De la Cruz wameipa Uruguay ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Brazil, mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 jana, huku Neymar akilazimika kuondolewa kipindi cha kwanza baada ya kuumia kifundo cha mguu.

Nunez alianza kufunga dakika ya 42 kwa mpira wa kichwa na usiku wa Brazil ukazidi kuwa mbaya dakika mbili baadaye Neymar aliumia wakati akigombea mpira na De la Cruz.

Akiwa na huzuni, Neymar aliondoka uwanjani kwa machela baada ya kupokea matibabu kwa dakika kadhaa.

FA ya Brazil ilisema kuwa fowadi huyo alikuwa na maumivu mkali ya goti la kushoto na kwamba atafanyiwa vipimo ili kubaini kama kuna shida zaidi.

“Hebu tutumaini sio jambo kubwa,” nahodha wa Brazil Casemiro aliambia televisheni ya Globo.

“Ni mchezaji muhimu kwetu, tunampenda sana. Amekuwa akisumbuliwa sana na majeraha na anapoanza kurudi kwenye uwezo wake anaumia tena.”

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *